Jina la Kitabu: فضل الإسلام (Fadhila za Uislamu)
Mwandishi: Shaykh Muḥammad bin ʿAbd al-Wahhāb رحمه الله
📝 Maelezo
Kitabu hiki kinaeleza juu ya ubora na fadhila kubwa za Uislamu, na namna Uislamu unavyowainua wafuasi wake pale wanaposhikamana na mafundisho yake. Shaykh Muhammad bin ʿAbd al-Wahhāb ameonesha kwa dalili kutoka Qur’an na Sunna kwamba dini ya Uislamu ndiyo njia sahihi ya mafanikio katika dunia na Akhera.
Kitabu pia kinatahadharisha dhidi ya kuacha Sunnah na kuingiza mambo ya bid‘a na shirki, ambavyo hupunguza thamani ya Uislamu wa mtu na kumweka katika hatari ya kupotea.
Sheikh Shahid Muhammad hufundisha kitabu hiki kila Jumatatu na Alhamisi katika Masjid Abeid, Mwanza, na hufafanua kwa lugha ya Kiswahili kwa kutumia mifano halisi ya maisha ya kila siku. Kusikiliza darsa hizi ni fursa ya kujifunza na kufaidika zaidi na mafunzo ya kitabu hiki.