AQIDAT
AHL AL-SUNNAH WA AL-JAMA'AH
AQIDA YA AHLUS-SUNNAH WAL-JAMA‘AH –SHEIKH: IBN ‘UTHAYMIN رحمه الله
Kitabu hiki kinabainisha misingi ya itikadi sahihi ya Uislamu:
• Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika ibada, majina na sifa Zake.
• Kusadikisha Qur’an kuwa ni maneno ya Allah.
• Kumfuata Mtume Muhammad ﷺ kama Mtume wa mwisho.
• Kuamini Malaika, Mitume, Vitabu, Siku ya Mwisho na Qadar.
• Kuwapenda Maswahaba na kushikamana na Jama‘a ya Waislamu.
• Kuepuka bid‘ah na kushikamana na Qur’an na Sunnah.
Kitabu hiki kimesomeshwa na Sheikh Shahid Muhammad ndani ya Masjid Abeid – Mwanza, katika darsa za Jumatatu na Jumatano kuanzia mwaka 2023 hadi 2024.
Katika audio za darsa hizi, Sheikh amefafanua kwa kutumia mifano halisi ya maisha ya sasa, na kuzifungamanisha dalili za Qur’an na Sunnah na matukio ya kila siku, kwa lugha nyepesi ya Kiswahili inayoeleweka kwa wote.